SIMULIZI YA DADA YANGU SURA YA 7
KITABU MALIPO NI HAPAHAPA
MTUNZI ADELA DALLY KAVISHE
MTUNZI ADELA DALLY KAVISHE
Ilipoishia........
“Juliasi karibu utaondoka kwenda Dar hivi kweli utanikumbuka? Na jinsi
warembo walivyo wengi huko Dar?” Aliuliza Esta huku akimpapasa uso
James.
“Hapana
siwezi kukuacha mpenzi wangu tutawasiliana usijali. Arusha nitakuja
hata wewe utakuwa unakuja Dar es Salaam.” Alijibu James huku akimbusu
Esta katika shavu la upande wa kushoto.
“Sawa
hakuna tatizo mimi naomba tuendelee kuwasiliana nakupenda sana mpenzi
wangu.” Alijibu Esta huku akiwa amemkumbatia na kumbusu James.
******************
Inavyoendelea.....Huko
Dar es Salaam Upendo alikuwa anaandaa mapokezi ya kumpokea mchumba wake
James ambaye walikuwa hawajaonana yapata miezi minne. Alifanya usafi wa
mazingira ya nyumba na kubadilisha baadhi ya vitu ili kuonekane
tofauti. Alikuwa na furaha sana siku hiyo ambapo kesho yake James ndiyo
alikuwa akirud.i Alinunua maua mazuri ya rangi nyekundu pamoja na
mvinyo. Kesho yake James alirudi, Upendo alikwenda kumpokea uwanja wa
ndege yapata saa moja jioni. James alishuka kwenye ndege na kuelekea
sehemu za mapokezi na kumkuta Upendo aliyempokea kwa furaha sana.
“Darling (mpenzi) umependeza sana, umezidi kuwa mweupe, nimefurahi sana kuwa nawe tena” Aliongea James huku akiwa amemkumbatia Upendo.
“Yaani James nimefurahi sana umerudi nilikuwa mpweke sana.” Alijibu Upendo huku akimpokea James begi.
Walielekea
Kinondoni nyumbani kwa James. James alishangaa sana kuona mabadiliko ya
nyumba yake na jinsi ambavyo Upendo alikuwa amepamba.
“Mpenzi
unafaa sana katika mambo ya upambaji nyumba imekuwa tofauti kabisa
nimefurahi kweli wewe ni mke mzuri.” Aliongea James kwa furaha huku
akikaa kwenye sofa.
“Asante
mpenzi wangu nenda ukaoge uje tule chakula halafu unipe habari za
Arusha.” Upendo alimsihi James. Usiku ule ulikuwa ni usiku wa furaha kwa
wote wawili walikula na kunywa na kulala huku wakiwa na mikakati ya
kufunga ndoa haraka.
Hatimaye
maandalizi ya kumuaga Upendo yalikamilika na wakati huo wazazi wa James
walikuwa wakiandaa harusi. Mawasilianao ya Esta na James yalipungua
sana. Kila Esta akimpigia simu alikuwa akimdanganya kuwa ametingwa sana,
kitu ambacho kilikuwa kikimuumiza sana Esta. Hata hivvyo Esta
aliendelea kujipa moyo kuwa Juliasi anampenda bila kujua kuwa alikuwa ni
tapeli wa mapenzi. Baada ya miezi miwili kupita Esta aliugua homa na
kwenda hospitali ambapo alipimwa na kukutwa akiwa na ujauzito wa miezi
miwili. Kutokana na hali hiyo Esta alichanganyikiwa sana.
“Mungu
wangu nina mimba ya Juliasi nitafanyaje mimi na huyu mwanamume sijui
ana mpango gani na mimi. Nafikiria kuitoa mimba lakini naogopa sana.
Hapana lazima nimfahamishe hali halisi kwa sababu sijui nifanyeje. Kwani
nyumbani baba akijua ataniua na ndugu zangu watanifikiriaje, nikifika
chuo ni lazima nimpigie simu leo.” Aliwaza Esta huku machozi
yakimlengalenga
Esta
aliondoka pale hospitali akiwa na mawazo mengi sana. Alipofika chuoni
aliingia chumbani kwake na kupiga simu. Simu iliita muda mrefu bila
kupokelewa. Aliendelea kupiga kama mara mbili bila mafanikio hadi
alipojaribu tena ndipo simu ilipokelewa na James aliyekuwa kazini kwake
muda huo.
“Haloo vipi Juliasi mbona nakupigia simu yangu hupokei?” Auliza Esta.
“We
mwanamke mjinga kweli inamaana niache kazi zangu nipokee simu yako? Je,
hujui kwamba huu ni muda wa kazi? Je, unasemaje?” Aliuliza James kwa
sauti iliyojaa hasira .
“Samahani
mpenzi kwa usumbufu nimekupigia nikwambie leo nimekwenda hospitali
kupima nina mimba yako ya miezi miwili.” Esta alimfahamisha James. “Hee!
Nini? Mimba! Ya nani!” Alihamaki James huku akionyesha kama mtu
aliyekanganyikiwa.
“Kweli
Juliasi unaweza kuniuliza kuhusu mimba hali unajua ni yako? Halafu
unaniuliza ya nani?” Aliuliza Esta huku amebana pua kumuigiza James.
“Sikiliza
nikwambie Esta, mimi sina mpango wa kuwa na mtoto sasa hivi, kama wewe
ulitaka mtoto ni juu yako ninachoweza kukusaidia ni pesa ya kutoa hiyo
mamba.” Alisema James kwa sauti ya kutetema tofauti na siku nyingine.
Esta hakuamini maneno anayoambiwa na James”
“Sikujua
kama utanifanyia hivi Juliasi, unajua ni kiasi gani nakupenda,
nashukuru sana ila hii mimba sitaitoa na huyu mtoto ni wako na nitamleta
huko huko Dar es Salaam.” Kisha akakata simu na kulia kwa uchungu huku
akijilaumu moyoni mwake na kujipa matumaini”
“Nilijua
Juliasi ni mwanaume mkweli kumbe yuko hivi au kwa sababu ya hii mimba
imekuja ghafla, sijui nifanyeje naamini mambo yatakwenda sawa, ngoja
nimwache kwanza kwa sasa.” Alijipa moyo Esta.
Esta aliendelea kuwaza sana na baadaye akamua kuendelea na shughuli zake za kawaida.
James naye alibaki akiwaza moyoni mwake.
“Hivi
nimefanya nini mimi huyu msichana ana mimba yangu na hataki kuitoa na
mimi nafunga ndoa hivi karibuni. Sijui itakuwaje ila ngoja nimwache
siwezi kumpoteza Upendo nampenda sana na ndio mke wangu, sitaki
mawasiliano na huyu mwanamke tena.”
Basi
naye aliendelea na mambo yake huku akiwa anajiandaa na harusi yake.
Wakati huo Upendo alipanga safari ya kwenda Morogoro kwani ilikuwa
imebaki kama mwezi mmoja afanyiwe sherehe ya kuagwa na wazazi wake.

No comments:
Post a Comment
Never Ever fuck with me got it men by @#619innoweezy