INNOWISE INFORMATION.Inc
WELCOME TO MY BLOG www.innowise-infor.com imethaminiwa na EPSON Company associated with CISCO LABS
Black Album
Wednesday, November 7, 2012
Hii budy back in tanzanian now u can contact me any time,ask any thing in my power I can help u.thanks for following my website and bloggs and so much for u to come.......
| Reactions: |
Tuesday, May 15, 2012
UtandaRhymes: War On Terror
Colonialism, similarly to slavery, divided Africans, planting
a seed of self-hatred. Today’s classism is no different from that,
thanks to our greedy leaders. These African leaders that perpetuate
this, terrorizing their own people, cannot possibly be from our Africlan, but from the AfriKKKlan.
War on corruption is probably the longest fought war in Africa. Similarly to war on terror, there doesn’t seem to be a clear end in sight for both of these wars. War on terror however, the attacks have been both ways between the terrorists and the West. But what have the have-nots done to the elite class, for them to allow corruption and bad governance to continue hurting the poor?
War on corruption is probably the longest fought war in Africa. Similarly to war on terror, there doesn’t seem to be a clear end in sight for both of these wars. War on terror however, the attacks have been both ways between the terrorists and the West. But what have the have-nots done to the elite class, for them to allow corruption and bad governance to continue hurting the poor?
| Reactions: |
Sunday, May 13, 2012
Simba wakomaaa kiume uko Sudan
SIMBA SC imeshindwa kutimiza ndoto za kusonga mbele kwenye Kombe la
Shirikisho la Soka Afrika, baada ya kutolewa kwa penalti 9-8 na Al Ahly
Shandy ya Sudan kufuatia sare ya jumla ya tatu.
Katika mchezo huo, uliofanyika kwenye Uwanja wa Shandi, penalti za
Shandy zilifungwa na Razak Yakubu, Orwa, Bashir, Saddam, Isaac Seun
Malik, Faris Abdallah, Fareed Mohamed Zakaria Nasu na kipa Abdulrahman
Ali.
Waliofunga penalti za Simba ni Felix Sunzu, Salum Machaku, Emanuel Okwi,
Shomari Kapombe, Kelvin Yondan, Victor Costa, Mwinyi Kazimoto na Amir
Maftah.
Eltigani alikosa kwa upoande wa Shandy wakati Mafisango na Kaseja
walikosa. Aliyeihakikishia Simba kutpolewa alikuwa ni Nahodha Kaseja,
ambaye alikosa penalti ya 10.
Shandy waliingia kwenye mchezo wa leo, wakiwa nyuma kwa 3-0 kutokana na
ujshindi wa SImba kwenye mechi ya kwanza, Dar es Salaam.
Hadi mapumziko, hakuna timu iliyokuwa imeona lango la mwenzake na hiyo
ilijenga matumaini kwamba, SImba itasonga mbele, lakini kipindi cha pili
mambo yalibadilika mno.
Mabao mawili ya Fareed Mohamed katika za 46 na 64 na lingine la Hamouda
Bashir dakika ya 50, yaliisaidia Al Ahly Shandy kushinda 3-0 na kufanya
sare ya jumla ya 3-3, baada ya dakika 180 za mechi mbili.
Lawama zote zimuendee beki Victor Costa kwa kufungisha mabao mawili-
hususan la pili na la tatu ambalo dhahiri yalitokana na ‘ubishoo’ wake
usio na maana.
Hii inahidhirisha mchezaji huyo aliyepangwa kwa dharula leo, kocha
Milovan Cirkovick alikuwa hakosei kutompanga- kwani leo ameigharimu timu
na haijulikani kwa nini apangwe yeye badala ya Obadia Mungusa.
| Reactions: |
Saturday, May 12, 2012
AJali ya basi lililoungua moto juzi Mji kasoro Bahari(Morogoro)
Bus la kampuni ya MURO investment lenye namba za usajili T820 BEY juzi liliteketea kwa moto mkoani Morogoro. Habari zinasema kuwa chanzo cha moto huo ni hitilafu ya umeme iliyojitokeza katika bus hilo, hata hivyo hakuna abiria yeyote aliyepata madhara kutokana na moto huo isipokuwa mali zote za abaria ziliteketea ndani kwa moto.
| Reactions: |
SIRI KUBWA YAFISHUKA,BABA NDIE ALIYETOBOA HAYO
Akizungumza kwa njia ya simu wikiendi iliyopita kutokea Shinyanga, Mzee Kusekwa alisema wanaomtuhumu kuhusika na kifo cha mwanaye wanakosea kwa vile kuna jambo jingine nyuma ya pazia.
MWANZO WA JAMBO LENYEWE
“Ni vigumu kwa mtu ambaye una mtoto mkubwa unayemtegemea katika maisha halafu ushiriki kumfanyia mambo ya kishirikina, hilo haliwezekani hata siku moja.
“Watu wanatumia kigezo cha kuhitilafiana na mwanangu kuwa sababu ya kunihusisha na kifo chake. Yule ni mwanangu hata iweje, mtoto akikuchafua mkono kwa kinyesi huwezi kuukata mkono, hayo yalishapita sioni sababu ya kutaka kuhusishwa na kifo hicho.”
AANZA KUFUNGUKA
Akienda mbali zaidi, mzee huyo alisema tatizo lilisababishwa na tambiko ambalo yeye aliliita haramu kwa sababu halikuwahusisha wazee wa kimila wala kufuata taratibu zinazotakiwa.
Alisema, tatizo ni kijana aitwaye Ayubu Mujungu ambaye ni mpwa wake (mtoto wa dada yake mzee huyo) aliyemchukua marehemu Kanumba na kumpeleka kwenye kaburi la babu yake kutambika kinyume na utaratibu wa mila zao.
“Kama ni matatizo ameyasababisha Ayubu ambaye kwa ujeuri tu alimchukua marehemu na kumpeleka Simiyu kwa ajili ya kutambika katika makaburi ya wazazi wangu.
“Binafsi miye na wazee wenzangu tulishangaa kuona kijana huyo akimchukua mtoto mwenziye (Kanumba) na kwenda naye kutambika katika makaburi bila ya kuwajulisha wazee.
“Kikwetu suala la matambiko hufanywa kwa taratibu maalum tena chini ya usimamizi wa wazee. Siyo mtu yeyote anaweza kwenda kufanya tambiko,” alisema.
ALIKIUKA MASHARTI
Alisema jambo jingine linalomfanya ahusishe tambiko la Kanumba na Ayubu katika kifo hicho ni kitendo cha marehemu kukiuka masharti ya kufanya tambiko kwa kuvaa mavazi siyo.
“Kuna kosa lingine Kanumba alilifanya, alivaa nguo nyeusi ambazo wazee wanasema kuwa haziruhusiwi kwenda nazo huko,” alisema.
Mzee Kusekwa alisema kuwa matokeo ya kukiuka mavazi, baada ya Ayubu na Kanumba kufika makaburini walikutana na vitu vya ajabu ambavyo mpaka leo ni Ayubu tu ndiye anayevijua lakini hataki kuviweka wazi.
Alizidi kuweka wazi kuwa ili kuwafunga midomo watu waliokuwa kwenye eneo la makaburi na kushuhudia maajabu yaliyowatokea wawili hao, waliwapa shilingi laki moja ili wasiseme.
“Hicho ndicho kilichosababisha kifo cha Kanumba kwa kuwa walikwenda kufukia vitu kwenye kaburi. Baada ya tukio lile mwanangu aliporejea Dar ndiyo akapata matatizo,” alisema.
KUHUSU MALI ZA KANUMBA
Mzee Kusekwa alisema muda wowote wiki hii atatua jijini Dar es Salaam kufuatilia suala la mali za mwanaye ambazo anadai amesikia zimeanza kuuzwa kiaina.
“Kuna kesi nimefungua Mahakama Kuu kuhusu kuzuia mali za mwanangu kuuzwa, hilo ndilo haswa linalonileta Dar. Kuna watu wanasema eti kwa mila za Kisukuma sistahili kuwa mrithi kwa sababu sikumtolea mahari mama Kanumba, hao wanakosea sana.
“Duniani kote watu wameshindwa kufananisha thamani ya fedha na uhai wa mtu, hakuna anayejua thamani ya mbegu ya Kanumba, hivyo kama sikumtolea mahari mama yake siyo sababu ya kunizuia kurithi mali za mwanangu. Mimi ndiye msimamizi wa mirathi,” alisema.
AMCHAMBUA AYUBU
Mzee Kusekwa alisema, chokochoko zote hizo amezileta Ayubu ambaye ni mtoto mdogo, akasema yeye (Ayubu) hajui mzee huyo na mama Kanumba walikutana wapi na walioana au hawakuoana.
Ameongeza kuwa Ayubu ni mtu wa kuchunga sana kwa kuwa tayari ameshajipendekeza kwa mama wa marehemu ili atajwe kama msimamizi wa mirathi wakati si mtu wa ukoo wao.
AMSHAURI MAMA KANUMBA
Katika kile kilichoonekana kutuliza hali ya hewa, mzee Kusekwa alitoa maneno aliyosema kuwa ni ushauri kwa mzazi mwenzake, Flora Mtegoa.
“Namsihi mzazi mwenzangu asisikilize maneno ya Ayubu maana ni mchonganishi, sisi tulishafanya kikao cha wanandugu lakini hakutokea, tukamtafuta na polisi kutokana na maneno yake akajificha uvunguni, bahati mbaya hatukuwa na hati ya kuingia ndani,” alisema na kuongeza:
“Aache kuamini ushirikina kwa kusema mtoto amechukuliwa msukule, hakuna msukule hapo ni matatizo ya tambiko. Kikubwa kwake kwa sasa ni kujenga imani kwa Mungu kwa kuwa ndiye aliyemchukua kiumbe wake.”
AYUBU KIKAANGONI
Risasi Mchanganyiko lilimtafuta Ayubu kwa njia ya simu na kuzungumza naye kuhusiana na madai hayo ya mjomba wake ambapo alitoa ushirikiano wa kutosha.
Kwanza, alianza kwa kukiri kuongozana na merehemu Kanumba kwenye makaburi yanayozungumziwa, akasema aliyewaagiza kufanya hivyo ni mama wa staa huyo Bi. Mtegoa.
“Tangu mwaka jana, mama Kanumba aliniagiza nimpeleke ndugu yangu katika makaburi na siyo kutambika bali ni kwenda kuyafagilia, hivyo Machi mwaka huu ndiyo tukatimiza,” alisema.
Kuhusu kutokewa na kitu kibaya makaburini hapo, alikanusha ingawa alikiri kumpatia fedha dada yake anayemfuata aitwaye Lucy ambaye ni mlemavu wa miguu.
“Hatukuwa tunamhonga, hapana. Yule ni dada yangu, tena anayenifuata mimi, tuliamua kumpa fedha kwa ajili ya kujikimu. Hata hivyo si laki moja kama alivyosema mjomba, ilikuwa ni shilingi 80,000.
“Tena nakumbuka mimi nilitoa 50,000 na Kanumba akatoa 30,000 fedha ambazo hazikuwa na sharti lolote lile.”
KUHUSU KANUMBA KUVAA NGUO NYEUSI
“Kanumba alivaa suruali ya jeans, rangi siikumbuki vizuri lakini haikuwa nyeusi na shati la rangi ya kaki. Hakuvaa nguo nyeusi kabisa.”
Madai ya mzee Kusekwa kuwa anajipendekeza ili awe mrithi wa mali za marehemu Kanumba, Ayubu alisema si ya kweli na kwamba amejijenga vizuri kimaisha na si kutegemea mali za urithi.
“Nina pikipiki, gari, nyumba na ninaendesha biashara zangu mwenyewe, sina shida na mali za marehemu. Kwanza nafahamu kuwa mwenye haki ya kurithi ni mama mzazi wa Kanumba.
“Hata huko kuondolewa katika ukoo ni watu wachache tu waliokutana kutokana na ushawishi wa baba Kanumba na sijapewa taarifa yoyote kwa kuwa aliyepangwa kuniambia, Elius Meshack hajaniambia chochote mpaka sasa.”
Ayubu alisema anashukuru kuwa yeye amemzika ndugu yake, amemuona kwa mara ya mwisho wakati alipomvalisha nguo na kumuwekea Biblia katika jeneza lake.
Adela dairly Mitikaso Dj Choka the master production InnoWise Foundation
| Reactions: |
Friday, April 20, 2012
forty fun house
![]() |
| awakweli wabunifu |
![]() |
| enzi za mwalimu |
![]() |
MANCHESTA YUNAITED CLASS OF 2011-2012 |
Kulikuwa na class of 92 enzi hizo za kina paulo scholesy,David beckham,ryan giggs na wengineo,soccer pundit mmoja anaitwa Alan Hansen akamwambia Ferguson kuwa ''YOu will win nothing with kids'' huo ulikuwa mwaka 95-96.msimu huo manchester wakatwaa taji na mwaka unaofuatia,sasa je hii class of 2011 ya babu fergie
toto bishi hili

MZEE WA SAFARI NAONA ANATAKA KUTOA COLLABO NA SENTI 50
![]() |
kumekuwa na tetesi kuwa will smith aka big will style ame split na mkewe jada smith pinket,lakini wanandoa hawa ambao nimiongoni mwa couple wanaotengeneza pesa nyingi kwa mwaka wamekanusha hiyo kitu!
| Reactions: |
Tuesday, April 17, 2012
TANZANIAN MUSIC AWARDS 2012
HAWA NDO WASHINDI WA KILI MUSIC AWARDS 2012.
1. WIMBO BORA WA RAGGAE.
-ARUSHA GOLD BY WARRIORS FROM EAST.
2. WIMBO BORA WA DANCE HALL.
- MANENO MANENO BY QUEEN DARLIN.
3. WIMBO BORA WA ZOUK RHUMBA.
- DUSHELELE BY ALI KIBA.
4.BORA WENYE VIONJO VYA KIASILI.
- VIFUU UTUNDU BY A.T-
5. WIMBO BORA WA TAARABU.
- NANI KAMA MAMA BY MASHAUZI CLASSIC ( AISHA MASHAUZI).
6. WIMBO BORA WA KISWAHILI.
- DUNIA DARAJA BY TWANGA PEPETA-
7. WIMBO BORA WA AFRO POP.
- HAKUNAGA BY SUMA LEE-
8. WIMBO BORA WA R&B.
- NUMBER ONE FAN BY BEN PAUL-
9. WIMBO BORA WA HIP HOP.
- MATHEMATICS BY ROMA-
10. MSANII BORA ANAECHIPUKIA.
- OMMY DIMPOZ (NAI NAI SINGER).
11. RAPA BORA WA BAND.
- KALIJO KITOKOLOLO-
12. MSANII BORA WA HIP HOP.
- ROMA MKATOLIKI-
13. WIMBO BORA WA KUSHIRIKISHWA.
- NAI NAI BY OMMY DIMPOZ FT. ALI KIBA-
14. WIMBO BORA WA AFRIKA MASHARIKI.
-KIGEUGEU BY JAGUAR-
15. MTUMBWIZAJI BORA WA KIKE.
- KHADIJA KOPA-
17. MTUNZI BORA WA MWAKA.
- DIAMOND-
16. MTUMBWIZAJI BORA WA KIUME
- DIAMOND-
18. MTAYARISHAJI BORA WA MAPIGO YA MUZIKI.
- MANEKE-
19. VIDEO BORA YA MWAKA.
- MAWAZO BY DIAMOND-
20. WIMBO BORA WA MWAKA.
- HAKUNAGA BY SUMA LEE-
21. HALL OF FAME.
- TAASISI JKT-
22. HALL OF FAME KWA MTU BINAFSI.
- KING KIKII-
23. HALL OF FAME KWA MTU BINAFSI.
- DR. REMMY ONGALA-
24. MWIMBAJI BORA WA KIKE.
- LADY JAY DEE-
25. MWIMBAJI BORA WA KIUME.
- BARNABA-
| Reactions: |
HAPPY BIRTHDAY ADELA
HAPPY BIRTHDAY TO YOU.
| kikazi zaidi |
| Message kutoka kwa ndugu jamaa na marafiki nazisomaje kwa umakini |
| Message nyingi naulizwa vipi Birthday utafanyia wapi |
| Nachatije |
| PEACE, Namshukuru sana Mungu kwa siku yangu ya kuzaliwa pia asanteni sana wadau wangu kwa kuwa pamoja nami wakati wote |
| HAPPY BIRTHDAY TO YOU |
Labels:
ALBUM YETU
SIMULIZI YA DADA YANGU SURA YA 7
KITABU MALIPO NI HAPAHAPA
MTUNZI ADELA DALLY KAVISHE
MTUNZI ADELA DALLY KAVISHE
Ilipoishia........
“Juliasi karibu utaondoka kwenda Dar hivi kweli utanikumbuka? Na jinsi
warembo walivyo wengi huko Dar?” Aliuliza Esta huku akimpapasa uso
James.
“Hapana
siwezi kukuacha mpenzi wangu tutawasiliana usijali. Arusha nitakuja
hata wewe utakuwa unakuja Dar es Salaam.” Alijibu James huku akimbusu
Esta katika shavu la upande wa kushoto.
“Sawa
hakuna tatizo mimi naomba tuendelee kuwasiliana nakupenda sana mpenzi
wangu.” Alijibu Esta huku akiwa amemkumbatia na kumbusu James.
******************
Inavyoendelea.....Huko
Dar es Salaam Upendo alikuwa anaandaa mapokezi ya kumpokea mchumba wake
James ambaye walikuwa hawajaonana yapata miezi minne. Alifanya usafi wa
mazingira ya nyumba na kubadilisha baadhi ya vitu ili kuonekane
tofauti. Alikuwa na furaha sana siku hiyo ambapo kesho yake James ndiyo
alikuwa akirud.i Alinunua maua mazuri ya rangi nyekundu pamoja na
mvinyo. Kesho yake James alirudi, Upendo alikwenda kumpokea uwanja wa
ndege yapata saa moja jioni. James alishuka kwenye ndege na kuelekea
sehemu za mapokezi na kumkuta Upendo aliyempokea kwa furaha sana.
“Darling (mpenzi) umependeza sana, umezidi kuwa mweupe, nimefurahi sana kuwa nawe tena” Aliongea James huku akiwa amemkumbatia Upendo.
“Yaani James nimefurahi sana umerudi nilikuwa mpweke sana.” Alijibu Upendo huku akimpokea James begi.
Walielekea
Kinondoni nyumbani kwa James. James alishangaa sana kuona mabadiliko ya
nyumba yake na jinsi ambavyo Upendo alikuwa amepamba.
“Mpenzi
unafaa sana katika mambo ya upambaji nyumba imekuwa tofauti kabisa
nimefurahi kweli wewe ni mke mzuri.” Aliongea James kwa furaha huku
akikaa kwenye sofa.
“Asante
mpenzi wangu nenda ukaoge uje tule chakula halafu unipe habari za
Arusha.” Upendo alimsihi James. Usiku ule ulikuwa ni usiku wa furaha kwa
wote wawili walikula na kunywa na kulala huku wakiwa na mikakati ya
kufunga ndoa haraka.
Hatimaye
maandalizi ya kumuaga Upendo yalikamilika na wakati huo wazazi wa James
walikuwa wakiandaa harusi. Mawasilianao ya Esta na James yalipungua
sana. Kila Esta akimpigia simu alikuwa akimdanganya kuwa ametingwa sana,
kitu ambacho kilikuwa kikimuumiza sana Esta. Hata hivvyo Esta
aliendelea kujipa moyo kuwa Juliasi anampenda bila kujua kuwa alikuwa ni
tapeli wa mapenzi. Baada ya miezi miwili kupita Esta aliugua homa na
kwenda hospitali ambapo alipimwa na kukutwa akiwa na ujauzito wa miezi
miwili. Kutokana na hali hiyo Esta alichanganyikiwa sana.
“Mungu
wangu nina mimba ya Juliasi nitafanyaje mimi na huyu mwanamume sijui
ana mpango gani na mimi. Nafikiria kuitoa mimba lakini naogopa sana.
Hapana lazima nimfahamishe hali halisi kwa sababu sijui nifanyeje. Kwani
nyumbani baba akijua ataniua na ndugu zangu watanifikiriaje, nikifika
chuo ni lazima nimpigie simu leo.” Aliwaza Esta huku machozi
yakimlengalenga
Esta
aliondoka pale hospitali akiwa na mawazo mengi sana. Alipofika chuoni
aliingia chumbani kwake na kupiga simu. Simu iliita muda mrefu bila
kupokelewa. Aliendelea kupiga kama mara mbili bila mafanikio hadi
alipojaribu tena ndipo simu ilipokelewa na James aliyekuwa kazini kwake
muda huo.
“Haloo vipi Juliasi mbona nakupigia simu yangu hupokei?” Auliza Esta.
“We
mwanamke mjinga kweli inamaana niache kazi zangu nipokee simu yako? Je,
hujui kwamba huu ni muda wa kazi? Je, unasemaje?” Aliuliza James kwa
sauti iliyojaa hasira .
“Samahani
mpenzi kwa usumbufu nimekupigia nikwambie leo nimekwenda hospitali
kupima nina mimba yako ya miezi miwili.” Esta alimfahamisha James. “Hee!
Nini? Mimba! Ya nani!” Alihamaki James huku akionyesha kama mtu
aliyekanganyikiwa.
“Kweli
Juliasi unaweza kuniuliza kuhusu mimba hali unajua ni yako? Halafu
unaniuliza ya nani?” Aliuliza Esta huku amebana pua kumuigiza James.
“Sikiliza
nikwambie Esta, mimi sina mpango wa kuwa na mtoto sasa hivi, kama wewe
ulitaka mtoto ni juu yako ninachoweza kukusaidia ni pesa ya kutoa hiyo
mamba.” Alisema James kwa sauti ya kutetema tofauti na siku nyingine.
Esta hakuamini maneno anayoambiwa na James”
“Sikujua
kama utanifanyia hivi Juliasi, unajua ni kiasi gani nakupenda,
nashukuru sana ila hii mimba sitaitoa na huyu mtoto ni wako na nitamleta
huko huko Dar es Salaam.” Kisha akakata simu na kulia kwa uchungu huku
akijilaumu moyoni mwake na kujipa matumaini”
“Nilijua
Juliasi ni mwanaume mkweli kumbe yuko hivi au kwa sababu ya hii mimba
imekuja ghafla, sijui nifanyeje naamini mambo yatakwenda sawa, ngoja
nimwache kwanza kwa sasa.” Alijipa moyo Esta.
Esta aliendelea kuwaza sana na baadaye akamua kuendelea na shughuli zake za kawaida.
James naye alibaki akiwaza moyoni mwake.
“Hivi
nimefanya nini mimi huyu msichana ana mimba yangu na hataki kuitoa na
mimi nafunga ndoa hivi karibuni. Sijui itakuwaje ila ngoja nimwache
siwezi kumpoteza Upendo nampenda sana na ndio mke wangu, sitaki
mawasiliano na huyu mwanamke tena.”
Basi
naye aliendelea na mambo yake huku akiwa anajiandaa na harusi yake.
Wakati huo Upendo alipanga safari ya kwenda Morogoro kwani ilikuwa
imebaki kama mwezi mmoja afanyiwe sherehe ya kuagwa na wazazi wake.
Umelala usiku mwenzio anachati au anatumia muda huo kuongea kwenye simu na mpenzi wake wa nje je wewe utafanyaje??
| Reactions: |
Subscribe to:
Posts (Atom)















































